Tuesday, September 25, 2012

Papaa On Tuesday......Kama Wengine Wanaweza Kwanini Mimi Nisiweze? | Sam Sasali a.k.a Papaa

Papaa On Tuesday......Kama Wengine Wanaweza Kwanini Mimi Nisiweze? | Sam Sasali a.k.a Papaa

Siku za Papaa on Tuesday ya Samuel Sasali kwangu huwa ni vituko. Imejirudia hii mara kadhaa hebu niseme la leo.
Nilikuwa na mkutano na wadhungu kujadili PhD development yangu. Infact no nimetoka mkutanoni saa hizi. Nimeamka kama saa 3 hivi asubuhi (kwa saa za huko TZ) moja kwa moja kituoni METRO nikadaka 51 ofisini. Nimefika ofisini nikaamua kidogo ninoe kiingereza kwa angalau kupigia simu watu kadhaa. Wakati naanza kufikiri nimpigie nani "Negotiation" ikaanza! Kuna jamaa yuko Norway, hajui kiingereza vizuri, nina rafiki yangu Uingereza, hapatikani kwa simu. Nikawaza kuna Mpare mmoja mji jirani (Mathew) kumbe yuko darasani not reachable. Nikatamni nimpigie papaa (maana kupiga simu huku ni cheap kuliko voda-voda bongo), nikasita maana angeniuliza "Umesoma Papaa yangu ya leo?" Nani anataka maswali magumu. Nikaamua nitafute tu hiyo Ön tuesday" wauu kukuta tu ile Tpic Sentensi ikanikumbusha 2002 naingia chuo kikuu kwa mara ya kwanza walikuja wale jamaa kututisha kuwa hapa chuoni kuna vichwa vitatu (Tundui, Utouh na Mbano) walivyokuwa wanayataja hayo majina wa MU mnakumbuka (siwezi kutaja nimeokoka na nampenda YESU). lakin nilichokumbuka ni tu "kama kuna watu wanapata supp na wengine wanafaulu, mi sijifunzi kwa walioshindwa bali kwa walioshinda" Sasa hiki ndicho kimenifanya nisome makala yote maana ina maudhui tofauti na mlengo wangu wa 2002 na leo ni 2012 (september 25) almost tarehe moja na ile jamaa walikuja kutupa huo umatemate wa mambo ya SUPP. Tarehe 25/09/2002 ilikuwa jumatano na tulikuwa orentation week ndiyo siku nilijipa wazo "Why nijifunze kwa walioshindwa?" Miaka kumi baadaye 25/09/2012 (jumanne), napata wazo jipya "Yaaa nijifunze kwa walioshindwa". Utadhani hili halina maana lakini lina maana tu kwa wenye kuwaza hivi.
1. Aliyenitisha kuhusiana na walioshindwa alikuwa mwanafunzi aliyekuwa mbele yangu mwaka mmoja (alikuwa second na "finalist" year nilikuwa "Fom one")
2. Aliyeleat wazo la kujifunza kwa walioshindwa, ana qualify kuwa "om one" wakati mimi ni "Finalist"
3. Mahusiano ya Mimi "Baba Xtina" na Papaa ni "Mwalimu na Mwanaunzi Pacha" kwa maana, yeye ni mwalimu wangu sasa na siku zote zijazo, lakini ni mwanafunzi wangu wa kwanza "Financial Management"
4. Miongoni mwa wale waliokuja 25/09/2002 pale "BLT" baadaye alikuja kuwa mwanafunzi wangu Masters akifanya M.Sc (AF) ya MU.
5. Nahisi Papaa alitakiwa kuwa mbele yangu MU na hasa ukizingati "Sarakasi" zake za kusoma shule sita kwa miaka minne (kama sikosei)

mwisho: Ufafanuzi. Mzumbe university kuna wanafunzi wa aina zifuatazo na nitalinganisha na mnavyowaita vyuo vingine
1. MU - "Form One" >>> kwingine "First years"
2. MU - "Second year" >> Kwingine "Second year"
3. MU - "Finalist" >>> kwingine "Thid year"
4. MU - "Wazee wa Masters">>> kwingine "Masters"
5. MU - "Viwango DUNI" >>> kwingine "Diploma na Cerificate"
Mwisho wa mwisho, niwatakie siku njema na niwatakie kazi njema. kila jumanne nasoma hii kitu "On tuesday" nilianzishaga yangu "KURUZI" umeme ukawa mgao likazima (Godwin alitabiri kifo chake kabla), Nikaja na "On friday" nikahojiwa "ITADUMU" hahahaha bado ipo, sasa nitakuja na "Reflection on POT" lakini tu Amani Paul Gaseri akimaliza assignment yake!! Popote mkimwona mwambieni.

Friday, August 24, 2012

IRINGA, SIASA, UCHUMI NA MAENDELEO

IRINGA, SIASA, UCHUMI NA MAENDELEO

Iringa mkoa ulioko kanda ya Nyanda za juu kusini una fursa na changamoto nyingi kwa ajili ya maendeleo yake kisiasa na kiuchumi. Kwa sasa unapozungumzia Iringa unajumuisha wilaya za Mufindi, Kilolo, Iringa Vijijini na Iringa Mjini, baada ya wilaya za Rudewa, Njombe na Makete kujitoa na kuunda mkoa wake wa Njombe.

Tumefurahi kwani kuundwa kwa mkoa mpya pamoja na kuonekana kama ni kujitenga lakini ni chachu ya maendeleo. Wakati maendeleo ya Njombe yanaitegemea sana Iringa (kwa miundombinu), Iringa inaitegemea sana Njombe kwa mifumo ya Biashara hivyo kufanya mikoa hii miwili ndugu kuwa na uhusiano wa karibu na muhimu sana.

Kulingana na utafiti uliowahi kufanywa na ofisi ya Mkuu wa mkoa Iringa (ya zamani) "Per Capita GDP" ilionyesha kuwa wilaya ya Iringa kuwa na wastani mdogo wa pato huku ile ya Njombe ikiongoza. Pia ilionyesha wazi kuwa wilaya za Njombe na Mufindi zana uzalishaji wa viwanda huku Iringa Mjini ikijikita katika utoaji huduma na Kilolo na Iringa vijijini zikjikita katika Kilimo. Kwa wastani wilaya zote zilionyesha kujihusisha na kilimo isipokuwa ringa mjini kwa kiasi kidogo.

Maendeleo ya Uchumi

Tunapozungumzia maendeleo ya kiuchumi tunagusa nyanja zote zinazoendesha maisha katika mfumo wa biashara, fedha, mitaji, watu na raslimali za asili. Iringa tuna kila kitu, tuna watu, mifumo mizuri ya biashara, mitaji na raslimali asili. kinachopungua kidogo ni jinsi ya kuoanisha haya yote ili kufikia katika lengo kuu hapa nitatoa mfano.

"Wakati huduma nyingi za hotel ziko Iringa Manispaa, vivutio vingi vya utalii wa nje viko nje ya manispaa mfano Milima Udzungwa, Masalia ya Isimila, Hifadhi ya Ruaha na kwingine. Hii ni fursa pekee ambayo inaweza kuongeza mzunguko wa fedha katika maeneo yote. Jambo gumu ni kuwa, Kule RUAHA NP kuna uwanja wake wa ndege na hivyo kulazimu ndege kwenda moja kwa moja jambo ambalo linafanya huduma Mjini zisipate wateja" Huu ni mfano ambao kama ukifanyiwa kazi vizuri basi hilo linaweza kuwa si tatizo.

Iringa kuna watu, vijana wenye nguvu ya kufanya kazi; Tatizo dogo tulilo nalo ni kutokuwa na mfumo wa ujengaji ajira binafsi badala yake karibu wote tunatazama ajira za mshahara jambo linalosababisha wengi tuwe nje ya Iringa kwa sababu ya uchache wa ajira za mshahara hapo. Ipo nafasi kwa kutumia mfumo wa habari na wana habari kufanya tafiti zenye kuweka mazingira bora ya biashara halafu kuwafanya vijana wabaki mkoani kwa ajira binafsi hasa wasomi wetu.

Maendeleo ya Siasa

Hapa tuna kila sababu ya kujivunia. Kwa leo sitaeleza sana ni mafanikio gani tumeyapata kama mkoa kwa kipindi kirefu. Rai yangu kwa wana Iringa ni kuona tuna nafasi ya kuaminiwa na tuna nafasi ya kujenga nchi yetu kwa taaluma zetu na nafasi zetu. Suala la msingi ni kuwa na mfumo wenye kuwezesha urithishaji wa moyo wa utumishi bora.

Wakati ujao tutaeleza kwa urefu mafanikio makubwa tuliyopata. Blog hii inaweza kukujuza mambo mengi, kaa karibu nayo!